Lango kuu la kuingilia katika kanisa la TPC kufuatia usanifu na upanuzi wa jengo la kanisa hilo.

Sanctus na Hosanna

Mtakatifu ni Mungu wetu, Bwana Sabaoth. Nchi yote imejaa utukufu wake.
Hosanna juu mbinguni. Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana.

Sala ya Shukrani

Mungu, tunakushukuru kwa ajili ya Yesu, ndugu yetu, uliyemfufua.
Ametangulia mbele yetu katika njia ya maisha, kifo na ufufuko.
Usiku wa mwisho wa maisha yake alifanya Pasaka pamoja na wale waliokuwa wake – ukombozi kutoka utumwani, tumaini la nchi mpya.
Alianzisha chakula ambacho tunasherehekea tena na tena kwa imani.
Chini ya ishara za mkate na divai anakuwepo.
Nguvu ya uhai wake itupitie na itufanye tuwe wamoja nawe na wamoja kwa pamoja.

Sala ya Kuomba Roho Mtakatifu na Maneno ya Kuanzishwa

Tunakushukuru, Bwana wa mbingu na nchi. Umewahurumia viumbe vyako na kumfanya Mwanao awe mwanadamu. Tunakushukuru kwa wokovu alioutimiza msalabani.
Tunakuomba:
Tuma juu yetu Roho Mtakatifu, utukasarishe mwili na roho, ili tupokee chini ya mkate na divai mwili na damu ya Kristo kwa wokovu wetu, tunapofanya aliyotuagiza.
Kwa maana Bwana wetu Yesu Kristo, usiku ule alipokuwa anasalitiwa, alitwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema:
Twaeni mle. Huu ni mwili wangu, unaotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.
Vivyo hivyo alitwaa kikombe baada ya chakula cha jioni, akashukuru, akawapa, akasema:
Twaeni mnywe wote, kikombe hiki ni Agano Jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu kwa ondoleo la dhambi. Fanyeni hivi, kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu.

 

Haupteingang der Kirche in TPC nach der Neugestaltung und Erweiterung des Kirchengebäudes.

Sanktus

Heilig ist unser Gott, der Herr Zebaoth. Alle Lande sind seiner Ehre voll.
Hosianna in der Höhe. Gelobt sei, der da kommt im Namen des Herrn.

Dankgebet

Gott wir danken dir für Jesus, unseren Bruder, den du auferweckt hast.
Er ist den Weg für uns vorausgegangen im Leben, Sterben und Auferstehen.
In der letzten Nacht seines Lebens hat er mit denen, die zu ihm gehörten, das Pascha gefeiert, die Befreiung aus der Abhängigkeit, die Hoffnung auf ein neues Land.
Er hat ein Mahl gestiftet, das wir glaubend immer neu feiern.
Unter den Zeichen von Brot und Wein wird er gegenwärtig.
Seine Lebenskraft durchströme uns und bewirke, dass wir verbunden sind mit dir und untereinander.

Epiklese und Einsetzungsworte

Wir loben Dich, Herr, des Himmels und der Erde. Du hast Dich über Deine Geschöpfe erbarmt und
Deinen Sohn Mensch werden lassen. Wir danken Dir für die Erlösung, die Er am Kreuz vollbracht hat.
Wir bitten Dich:
Sende auf uns herab den Heiligen Geist, heilige uns an Leib und Seele,
damit wir unter Brot und Wein Leib und Blut Christi zu unserem Heil empfangen,
wenn wir tun, was Er uns geboten hat.
Denn unser Herr Jesus Christus, in der Nacht da Er verraten ward,
nahm Er das Brot, dankte und brach’s und gab’s Seinen Jüngern und sprach:
Nehmet hin und esset. Das ist mein Leib, der für euch gegeben wird. Solches tut zu Meinem Gedächtnis.
Desgleichen nahm Er auch den Kelch nach dem Abendmahl, danke und gab ihnen den und sprach:
Nehmet hin und trinket alle daraus, dieser Kelch ist das Neue Testament (der neue Bund) in meinem Blut, das für euch vergossen wird zur Vergebung der Sünden. Solches tut, sooft ihr’s trinket, zu meinem Gedächtnis.