Desemba / Dezember 2026

Advento: Wakati wa Kumngojea Mfalme

Inakuwaje kwamba majilio yanaonekana kufaa kabisa kwa hali hii ya sherehe? Jibu la swali hili limejificha katika mapokeo ya kanisa. Kila Jumapili ya Advento ina lengo lake kuu yenyewe.

Katika Jumapili ya 1 ya Advento, lengo liko kwenye kuja kwa Yesu kama Mfalme. Jambo hili linakumbushwa na somo kuhusu Yesu kuingia Yerusalemu.
(Mathayo 21)

Jumapili ya 2 ya Advento inaelekeza mtazamo kwenye kuja kwa Kristo mara ya pili. Katika Jumapili hii, hotuba ya Yesu kuhusu nyakati za mwisho husomwa wakati wa ibada.
(Luka 21:25-33)

Katika Jumapili ya 3 ya Advento, waamini wanahimizwa kuandaa njia kwa ajili ya kuja kwa Yesu katika ulimwengu huu. Wakati huo huo, Yohane Mbatizaji anaangaziwa kwa wito wake wa toba.
(Luka 3)

Katika Jumapili ya 4 ya Advento, kumbukumbu ya pekee inaelekezwa kwa Maria. Anakubali kwa makusudi mapenzi ya Mungu na hivyo anakuwa mama wa Mwokozi anayekuja.
(Luka 1:26-56)

Jumapili za Advento zinasisitiza furaha ya kwamba Mungu analeta wokovu kwa ulimwengu huu kupitia Yesu.

Mzunguko huu wa sherehe za kanisa unatoa picha ya kwa nini nyimbo nyingi za Advento na Krismasi zina mwangwi wa kifalme na wa uhakika wa ushindi. Pamoja na liturujia, nyimbo hizi zinawakumbusha washiriki wa ibada kwamba Yesu ni Mfalme; kwamba siku moja ataondoa chanzo cha mateso na dhiki katika ulimwengu huu na kushinda ubaya wote kabisa.

Sisi wanadamu tunahimizwa kujiunga katika tumaini hili na katika vigelegele vya furaha vinavyojaza uumbaji wote.

 

Advent: Wartezeit auf den König

Woher kommt es, dass der Advent wie geschaffen scheint für diese festliche Stimmung? Eine Antwort auf diese Frage liegt in der kirchlichen Tradition verborgen. Jeder Adventssonntag hat einen eigenen Schwerpunkt.

Am 1. Advent liegt der Fokus darauf, dass Jesus als König kommt. Daran erinnert die Lesung vom Einzug Jesu in Jerusalem.
(Matthäus 21)

Der 2. Advent richtet den Blick auf die Wiederkunft Christi. An diesem Sonntag wird die Rede Jesu über die Endzeit im Gottesdienst gelesen.
(Lukas 21,25-33)

Am 3. Advent werden die Gläubigen aufgefordert, den Weg für die Ankunft von Jesus in dieser Welt vorzubereiten. Dabei steht Johannes der Täufer mit seinem Ruf zur Umkehr im Blick.
(Lukas 3)

Am 4. Advent erinnert man sich besonders an Maria. Sie nimmt den Willen Gottes bewusst an und wird so die Mutter des kommenden Heilandes.
(Lukas 1, 26-56)

Die Adventssonntage betonen die Freude darüber, dass Gott dieser Welt durch Jesus Rettung bringt.

Dieser kirchliche Festzyklus lässt erahnen, warum viele Advents- und Weihnachtslieder etwas Königliches und Siegesgewisses atmen. Gemeinsam mit der Liturgie erinnern sie die Besucher der Gottesdienste daran, dass Jesus König ist. Dass er die Ursache für Leid und Not einmal aus der Welt räumen und alles Böse endgültig besiegen wird.

Wir Menschen werden aufgefordert, in diese Hoffnung und in den Jubel einzustimmen, die die ganze Schöpfung erfüllen.